Sheria na masharti ya salio la ofa la utangazaji wa
mtandaoni yanatumika:
- Unastahiki kupata salio la ofa ikiwa (a) wewe ni
mtangazaji mpya kwenye Google Ads na onyesho lako la
kwanza la tangazo lilionyeshwa kutoka kwenye Akaunti
yako ya kwanza ya Google Ads katika kipindi
kisichozidi siku 14 kabla hujaweka msimbo wako wa
ofa; au (b) wewe tayari ni mteja wa Google Ads na
unawasha kipengele au bidhaa mpya kwenye Google Ads
au unafungua upya akaunti isiyotumika, kama
ilivyobainishwa na Google katika vocha. Masharti ya
kujiunga yanayotumika yamebainishwa katika ofa
unayopokea kutoka Google.
- Watangazaji watatozwa kwa utangazaji wote
unaozidi salio la ofa. Watangazaji wanaweza
kusimamisha matangazo yao wakati wowote kabla ya
kiasi cha salio la ofa kuisha ikiwa hawatapenda
kutozwa gharama za ziada za utangazaji. Watangazaji
hawataarifiwa mara tu salio la ofa litakapoisha.
- Mara tu matumizi na/au vitendo vinavyohitajika
kukamilika, ilimradi tu vigezo vyote vya kustahiki
vimetimizwa, kwa kawaida salio litawekwa ndani ya
siku 35 kwenye Muhtasari wa Malipo wa akaunti yako ya
Google Ads.
- Salio linaisha siku 60 baada ya kuwekwa kwenye
akaunti yako, isipokuwa ikibainishwa vinginevyo
katika sheria na masharti ya ziada ya ofa husika.
Unaweza kuangalia salio lako la ofa na tarehe za
mwisho wa matumizi kwa kuhakiki kichupo cha Ofa
kilicho chini ya ukurasa wa Malipo wa akaunti yako ya
Google Ads wakati wowote.
- Ofa inategemea idhini ya tangazo, usajili sahihi
na kukubalika kwa sheria na masharti ya kawaida ya
Mpango wa Google Ads.
- Salio la ofa haliwezi kuhamishwa na haliwezi
kuuzwa au kubadilishwa na bidhaa zingine.
- Ofa inaweza kubatilishwa na Google Ireland
Limited wakati wowote kwa sababu yoyote ile.
- Watangazaji wanawajibika na hawatakiwi kutumia
salio la ofa kulipa ya kodi zozote au ada zingine
zinazotozwa. Malipo ya kodi zozote au ada zingine za
Watangazaji hazitahesabiwa katika salio lolote la ofa
wanalopokea.
- Salio moja la ofa kwa mteja mmoja.
- Unatakiwa uwe umekusanya kiwango cha chini cha
gharama za utangazaji na kutozwa kikamilifu kabla ya
salio la ofa kuwekwa.
- Matumizi ya ofa yanaweza kutumika kwa chaguo za
malipo otomatiki pekee.
- Ukifungua akaunti yako ya Google Ads katika
sarafu tofauti na ile ambayo salio lako la ofa
limewekwa, kiwango halisi cha gharama za matumizi
pamoja na salio la ofa kinaweza kutegemea mabadiliko
ya thamani ya sarafu za kigeni.
- Ofa inatumika kwa wateja wenye anwani ya kutuma
bili pekee nchini Kenya.
- Ofa itaisha baada ya miezi 3 tangu maudhui yenye
vocha yalipotolewa kwa mara ya kwanza au tarehe ya
mwisho wa matumizi iliyo kwenye vocha (ikiwa ipo).
- Matumizi yako ya vocha hii na/au salio la ofa
inategemea na wewe kukubali kufuata sheria na
masharti haya. Ofa haitatumika ambapo hairuhusiwi
kisheria.
- Samahani kwa kukuelekeza kwa kutumia istilahi ya
kisheria!